Mambo 7 Yaliyojadiliwa Kwenye Mkutano Wa TAMONGSCO -August, 2023

Interview

Mambo 7 Yaliyojadiliwa Kwenye Mkutano Wa TAMONGSCO -August, 2023

1. Ujumbe na mwongozo kutoka kwa REO

REO,Bw. Abdul Mnonya alifungua mkutano na kutambulisha meza kuu ya walioalikwa kwenye mkutano huo uliofanyika Oysterbay katika ukumbi wa kanisa la St. Peters.  Pia alitoa mwongozo mzima wa jinsi kikao kitakavyoendeshwa na ratiba nzima ya mkutano.

2. Maelezo ya Msingi Kuhusu Service Levy na Zimamoto

  • Mwanasheria mshauri aliweza kutoa maelezo kuhusu service levy (ushuru wa huduma) kwa wawakilishi wa shule waliokuwepo kwenye mkutano kwamba kwa sasa ushuru ni wa huduma tu na sio wa majengo. Maswali mengi yaliulizwa na maoni yalitolewa kwa mwanasheria huyo ili kufikia muafaka katika eneo hilo.
  • Wawakilishi wa polisi pia waliweza kuwaeleza wenye shule umuhimu wa kufanya ukaguzi wa kushtukiza kwa wanafunzi kuepuka ajali za moto zinazopelekea hasara kubwa kwa shule.

3. Umuhimu wa Kutumia ShuleSoft kwa Shule za Tanzania

Eng Ephraim Swilla kutoka Shulesoft alieleza kwa ufupi umuhimu wa programu hii ya shule ambayo imesha ongeza ufanisi mkubwa kwa zaidi ya shule 400 Tanzania nzima zinazotumia mfumo huu.

Kwa ufupi Eng. Ephraim Swill alieleza faida zifuatazo

  • Kuongeza ufanisi wa ukusanyaji Ada kwenye Shule
  • Kuboresha na kurahisisha uandaaji wa matokeo kwa wakati
  • kuimarisha mahusiano na wazazi, hivyo kuongeza wigo wa kupata wanafunzi zaidi
  • kuimarisha usimamiaji wa wafanyakazi, kwa kujua ufanisi wao wa kazi kupitia system ya shulesoft
  • kupunguza gharama za uendeshaji wa shule kwa kuondoa ufanyaji kazi wa karatasi

Eng. Ephraim alieleza kuwa mfumo wa Shulesoft una moduli zifuatazo

 

  • Administration: Hapa Shule wanasajili wanafunzi, wazazi, walimu na wafanyakazi, kuandaa vitambulisho vya wanafunzi na staff, kuandaa ripoti za ufanisi za wafanyakazi (Performance reports), kupata ripoti mbalimbali za wanafunzi n,k.
  • Academic : Hapa shule huweza kusimia mitalaa ya walimu (syllabus), kuandaa matokeo kwenye mfumo kwa dakika chatu tu, shule nzima kupata matokeo na kuwatumia wazazi, kuandaa ripoti za NECTA (CA), kuandaa ripoti za ubora (qualitative reports) etc.
  • Accounts: Hapa shule huweza kuandaa invoice (control number), na kuzituma kwa wazazi, ku record matumizi ya shule (expenses, fixed assets, liabilities etc), kufanya ulinganifu (bank reconciliation), kuandaa mishahara (payroll), etc
  • Communications: Mfumo wa ShuleSoft umeunganishwa na Bulk-sms, Whatsapp, Telegram etc, hivyo kuleta urahisi sana kuwasiliana na wazazi
  • Operations: Hapa shule wanaweza simamia Maktaba, Mahudhurio, ratiba za shule, usafiri etc
  • Digital Learning : Hapa shule wanaweza fundisha wanafunzi pindi wanapokua likizo majumbani, kwani hii sehemu huwezesha shule kurusha vipindi mubarashara, kuweka maswali mtandani, na kuruhu wanafunzi kujisomea wakiwa nyumbani

Tazama kwa ufupi ujionee mfumo ulivyo

mfumo huu pia unakuja na App special kwa ajili ya mzazi inayoitwa Parent experience Experience. App hii pendwa kwa ma elfu ya wazazi, imekua moja kati ya App bora kabisa Africa, na inatumiwa na wazazi ndani na nje ya Tanzania

 

Tazama kwa ufupi ujionee App ya wazazi

4. Kuanzisha SACCOSS ya TAMONGSCO

Mwenyekiti wa Tamongsco Bw. Amani Lyimo alitoa mapendekezo ya kuanzisha SACCOS kwa ajili ya kikundi hiki cha wenye shule binafsi kuweza kuchangisha wanachama wa Tamongsco ili kuweza kulipia mikutano na kuweza kufanikisha mikutano yao kwa ujumla na kusaidiana.

5. Safari ya China

Benki ya NBC na kampuni ya GNM imeweza kufadhili mkutano na kusafiri kwenda China kwa kutoa mikopo ya hadi asilimia 70% kwa watakaoenda nchi hiyo. Madhumuni ya kwenda China ni kujenga mahusiano mazuri na wasambazaji wa bidhaa za shule ili waweze kupata  bidhaa hizo kwa gharama nafuu zaidi.

6. Insurance ya wanachama

Kampuni ya Jubilee insurance iliweza kutoa maelezo ya namna wanachama wake wanapata faida kwa kulipia bima hio. Pia Shulesoft pamoja na Sanlam insurance ina kipengele cha bima kinachomsaidia mzazi anapoumwa, kupata ajali au kufariki kuweza kumsomesha mwanao katika kipindi hicho

uzuri wa bima ya ShuleSoft, ni kwamba mzazi hulipa kiasi kidogo sana kati ya 10,000 hadi 30,000 kwa mwaka kutokana na Ada ya Shule, na pindi mzazi atapopatwa na changamoto, basi bima italipa ada ya mtoto tangu hilo darasa hadi anapo maliza shule, hivyo kuokoa gharama kwa shule pia

7. Uchaguzi

Kulikua na uchaguzi wa viongozi kuwakilisha shule kwa kila wilaya za kanda ya Dar es Salaam na kuweza kutoa matatizo na mrejesho kutoka kwa wanaowakilishwa. Kila wilaya ilifanikiwa kupata viongozi hao na huu ndo ulikua mwisho wa kikao hiki.

Kama kuna mengine tumeyaacha, usisite kuyaweka kwenye commnet hapo chini.

Play Now

More from Press

event image
Apr09
ShuleSoft Press

Taasisi ya ShuleSoft imezindua Mfumo mpya wa ShuleSoft unaojihusisha na usimamizi wa shule, ambapo imelenga kusaidia masuala ya utawala, taaluma, mamb

Read More