ShuleSoft Press

Interview

ShuleSoft Press

Taasisi ya ShuleSoft imezindua Mfumo mpya wa ShuleSoft unaojihusisha na usimamizi wa shule, ambapo imelenga kusaidia masuala ya utawala, taaluma, mambo ya kifedha, mawasiliano na kurahisisha ujifunzaji kwa mfumo wa kidigitali wa ShuleSoft.

Akizungumza na waandishi wa habari, Aprili 9, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa toleo jipya la mfumo huo, Mkurugenzi wa ShuleSoft, Ephraim Swilla amesema wamefanya maboresho ya mfumo huo kuongezea baadhi ya vipengele ambavyo havikuwepo awali kutokana na mapendekezo ya wateja wao.

Aidha, ameeleza kuwa toleo hilo jipya limeunganisha wadau mbalimbali zikiwemo benki na mitandao ya simu ambapo itarahisisha kutoa suluhu ya changamoto za malipo shuleni na kuokoa muda kwa utawala, wazazi pamoja na wanafunzi.

Amesema mfumo wa toleo hilo jipya la shulesoft unakwenda kusaidia, masuala ya usimamizi wa shule katika nyanja mbalimbali ambazo ni mahudhurio, maktaba, bweni, taaluma, mawasiliano ya moja kwa moja na wazazi pamoja na uwajibikaji wa wafanyakazi.

“Shule sasa wanaweza kusimamia mambo ya mahudhurio, maktaba, bweni lakini tuna kipengele cha kutuma mawasiliano kwa wazazi ambapo tumeuunganisha na Whatsapp, Telegram ikiwepo aplikesheni mpya ya simu inayoitwa (shule soft parent Experience) ambapo mzazi atajua kila kitu kinachoendelea shuleni,” amesema Swilla.

Pia, ametoa onyo kwa watu wanaoiba kazi za wabunifu nakufanya udanganyifu kwa shule na kuharibu ubunifu wao uliofanyika kwa kutumia jina la taasisi hiyo vibaya na kutengeneza taswira mbaya kwa jamii kwa kujiingizia mapato yasiyo halali.

Aidha, ametoa wito kwa wadau wote wa elimu kuungana kufikisha kileleni taaluma ya nchi hii katika viwango vya kimataifa na amewaalika wadau kutoka shule za umma na za binafsi ambazo hazijajiunga na mfumo huo wa shulesoft kufikia ofisi zao zinazopatikana Dar es Salaam, Arusha na Mbeya.

Mfumo wa toleo jipya la shulesoft umekusudia kuwaunganisha pamoja utawala wa shule, wazazi, pamoja na Wanafunzi ili kuboresha ujifunzaji katika kipindi hiki cha mageuzi ya sayansi na Teknolojia.

Akizungumzia mchango wa uwepo wa Taasisi hiyo katika kuchangiza elimu nchini, Swilla amesema kuwa wameweza kufikia zaidi ya shule 470 nchini ambazo wanafanya nazo kazi na wazazi zaidi ya 200,000.

“Pia tuna zaidi ya wanafunzi 200,000 wanaobnufaika na uwepo wa ShuleSoft huku tukifanya shughuli mbalimbali, kwani ukiangalia shule zetu nyingine zimeongeza utendaji kazi na hata ukusanyaji wa mapato umeon, gezeka kutoka wastani wa asilimia 60 hadi 70 lakini kupitia mfumo wetu wa ShuleSoft wameweza kufikia asilimia 90 na zaidi, hivyo mafanikio ni makubwa sana kufikia mfumo huu,” amesema Swilla.

Onyo kwa wanaochezea jina

Katika hatua nyingine Taasisi hiyo kupitia kwa Mwanasheria wa Taasisi hiyo, Faraja Msuya, imeonya mara moja kwa watu ambao walikuwa wakitumia nembo ya taasisi hiyo kufanya udanganyifu hatua ambayo ilikuwa ikiwarudisha nyuma.

Mwanasheria wa Taasisi hiyo, Faraja Msuya.

“Baada ya kuwapo kwa watu waliokuwa wakitumia jina letu, tulifungua shauri Mahakama ya Hakimu Kazi Kinondoni na tukashinda kesi, watu hao walijaribu kwebnda mahakama kuu lakini kutokana na sababu za kisheria wahusika hao waliamua kuondoa shauri hilo.

“Ifahamike kwamba siyo lengo la Shulesoft kuanza kukimbizana mahaakamlani na mdau yeyote wa elimu, lakini inapofika wakati unalazimisha, hakuna namna. Hivyo tulishinda hiyo kesi, na hatutaki kuendelea kuwa watu wa kesi licha ya kuwapo kwa watu ambao tulisha washinda kisheria lakini bado wanaendelea kudanganya kupitia majina tofautitofauti.

“Sasa licha ya onyo ambalo tulikuwa tayari tumetoa wengine walionyesha kukaidi, lakini sijui kama wanafahamu majina ya shule zao kutumika katika shughuli zisizo halali, sasa sisi mwisho wa siku tutalazimika kuchukua hatua kali dhidi yao kwani ni kazi ngumu kutengeneza chapa na kuikuza kisha watu waje waichezee,” amesema Mwanasheria Msuya.

Wanaochezea mfumo huo wanafanyaje?

Swilla amesema watu wanaochezea mfumo wao, kwanza wamekuwa wakichukua mifumo yao yaliyoanzisha kisha kwenda kwa wateja wakiwaambia kuwa ni wa ShuleSoft.

“Watu hao njia moja wanayoitumia kwanza wanakwenda kwa wateja na mfumo wao na kuwadanganya kuwa ni wa ShuleSoft hivyo wanawauzia kwa bei rahisi, hatua ambayo inawasukuma wateja kuona kwamba inapatikana kirahisi licha ya ukweli kuwa kuna kazi kubwa ya kufanya hadi kusimamisha ofisi.

“Mbinu ya pili watu hawa wametengeneza nyaraka za uongo wanazopita nazo kwa wateja wetu kisha kuwaambia kuwa ShuleSoft haifanyi kazi tena badala yake kuna kampuni nyingine jambo ambalo siyo kweli, hivyo wanatumia kila mbinu ili kuwashawishi wateja, kwa wateja albao hawajui kuhusu Teknolojia ni rahisi kudanganyika,” amesema Swilla.

Play Now

More from Press