YALIYOJIRI KATIKA MKUTANO WA WAZIRI WA ELIMU NA WAZIRI WA ELIMU NA WAMILIKI WA SHULE ZISIZO ZA SERIKALI

Interview

YALIYOJIRI KATIKA MKUTANO WA WAZIRI WA ELIMU NA WAZIRI WA ELIMU NA WAMILIKI WA SHULE ZISIZO ZA SERIKALI

Katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete, ulioongozwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda, akiwa na TAMISEMI. Mkutano huu ulikua wenye lengo la kupanga mikakati, kutoa changamoto na kuboresha shule binafsi. Yafuatayo ni machache ya yaliyoongelewa;

  1. Matumizi ya tehama

Wamiliki wa shule zisizo za serikali wamepata kujua umuhimu wa kutumia mfumo wa tehama katika shule zao. Wamiliki hawa wameweza kujua zaidi baada ya kupita kwenye banda la Shulesoft na kupata elimu juu ya mfumo wa kidigitali. Mfumo huu, unasaidia katika kupunguza shughuli za uendeshaji wa shule kwa kuwa na vipengele kama taaluma, uhasibu na mawasiliano. Hivyo kupelekea kuimarisha mahusiano mazuri kati ya shule na wazazi, kupunguza gharama ya uendeshaji shule na kukuza ufaulu wa shule.

  1.  Pongezi

Wamiliki wa shule binafsi wametoa pongezi zao kwa Waziri, kuita kikao ili kujua shida za shule hizo na kujua namna ya kutatua changamoto hizo.

  1. Kodi na tozo mbalimbali

Wawakilishi wa wamiliki wa shule walioweza kuongelea swala hili walisema kwamba tozo za huduma na majengo zisamehewe kwani wanatoa huduma ya elimu kama shule za serikali tu ambazo hazitozwi kodi hizi. Pia wanaokuja kwa ajili ya ukaguzi mbalimbali hapo shuleni wameombwa waache kuwawekea vitisho na ukatili kwa wenye shule binafsi mfano zimamoto.

  1. Utekelezaji wa sera na mitaala mipya

Wamiliki wa shule zisizo za serikali wametoa ombi la kuanzisha masomo ya amali kuanzia madarasa ya awali ili kuwaandaa wanafunzi tangu wakiwa wadogo. Pia wamesema walimu wa masomo haya wanatakiwa waandaliwe ili wawepo kwa wingi kwa ajili ya wanafunzi watakaokuwa wanasoma masomo haya vyuoni. 

  1. Maadili 

Kati ya maoni yaliyotolewa na wamiliki wa shule zisizo za serikali ni suala la kurudisha somo la dini katika shule na kupewa uzito sawa na masomo mengine. Hii ni kwa sababu wanafunzi hawaipi umuhimu maana somo halijapewa kipaumbele kama mengine kwenye mitihani. Somo hili la dini limeombwa lifundishwe kuanzia madarasa ya awali ili kuwalea watoto katika misingi iliyo bora.

  1. Bima

Shule za binafsi zimetoa ombi kwa serikali kutafuta namna ya watoto hawa kupata bima ya afya wakiwa shuleni. Hii ni kwasababu shule zisizo za serikali hutegemea mapato kutoka kwa wazazi na pindi mzazi anaposhindwa kulipa ada na huduma nyingine za shule wanafunzi kushindwa kuendelea na masomo kwa sababu shule haiwezi kumudu gharama hizo.

  1.  Miundombinu 

Maeneo mengi ya shule binafsi zina barabara mbovu kufikia shuleni. Wamiliki wa shule      wametoa ombi kwa serikali kwamba waawasaidie kuwatengenezea barabara zao ili kusadia watu kufikia shule hizo kwa urahisi muda wowote. Waziri akajibu kwa kusema atakaa na viongozi wa maeneo wakati wa kutoa huduma itoe kipaumbele kutoa huduma za umeme,maji na barabara kwenye sehemu za taasisi binafsi na umma.

Waziri Mkenda alihitimisha kwa kusema kwamba ameyapokea maoni na malalamiko yote na kuahidi kuyafanyia kazi kabla ya kukutana mwezi Machi mwakani 2024 kupata marejesho ya watakapokua wamefikia. Waziri pia alisema atafanya namna ya kuwapa shule hizi uhuru kwenye utoaji wa ajira na tozo za ada. Pia alitoa pongezi kwa wamiliki wa shule zisizo za serikali kwa kuwa wavumilivu na wakarimu kwake.

 

Mwisho, Shulesoft inapenda kuwajulisha kuwa tumeweza kuanzisha bima ya wanafunzi wa shule binafsi kwa wanafunzi waliofiwa na mzazi au mlezi, mzazi kuumwa na kushindwa kumhudumia mwanae na ajali inayomkwamisha mzazi kumhumdumia mwanae. Makundi yote haya yanaweza kusaidiwa kufanikisha ndoto zao za elimu kwani bima hii itamsomesha mwanae mpaka atakapomaliza ngazi hio ya elimu.

ShuleSOft Insurance

Karibu !!           

Kwa maelezo zaidi tupigie +255 748 771 580

Play Now

More from Press

event image
Apr09
ShuleSoft Press

Taasisi ya ShuleSoft imezindua Mfumo mpya wa ShuleSoft unaojihusisha na usimamizi wa shule, ambapo imelenga kusaidia masuala ya utawala, taaluma, mamb

Read More