Training & Support

Explore upcoming training sessions and past events to get the most out of ShuleSoft

Upcoming Events

No upcoming training sessions

Past Events

Academic refresher training:

event

Academic refresher training: Join and learn how to prepare Academic Reports that Parents, Students, and Management LOVE. This training is suitable for school academics and teachers. We will cover the following:1. Setting a system for effective reports2. Exam marking3. Single and Combined Exam report preparation4. How to engage parents to improve academic performance Friday, March 07th -2025 · 10:𝟬𝟬 – 11:𝟬𝟬h EAT Link: https://meet.google.com/xny-uspy-shc For more information, contact us: 𝟬𝟳𝟰𝟴𝟳𝟳𝟭𝟱𝟴𝟬 OR +255655406004 #Schoolmanagement #privateschools #Tanzania #elimubilamipaka #payroll #webinar #wizarayaelimu #shulesoftacademic #exams #SafariyaShuleSoft

ShuleSoft Press

press

Taasisi ya ShuleSoft imezindua Mfumo mpya wa ShuleSoft unaojihusisha na usimamizi wa shule, ambapo imelenga kusaidia masuala ya utawala, taaluma, mambo ya kifedha, mawasiliano na kurahisisha ujifunzaji kwa mfumo wa kidigitali wa ShuleSoft. Akizungumza na waandishi wa habari, Aprili 9, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa toleo jipya la mfumo huo, Mkurugenzi wa ShuleSoft, Ephraim Swilla amesema wamefanya maboresho ya mfumo huo kuongezea baadhi ya vipengele ambavyo havikuwepo awali kutokana na mapendekezo ya wateja wao. Aidha, ameeleza kuwa toleo hilo jipya limeunganisha wadau mbalimbali zikiwemo benki na mitandao ya simu ambapo itarahisisha kutoa suluhu ya changamoto za malipo shuleni na kuokoa muda kwa utawala, wazazi pamoja na wanafunzi. Amesema mfumo wa toleo hilo jipya la shulesoft unakwenda kusaidia, masuala ya usimamizi wa shule katika nyanja mbalimbali ambazo ni mahudhurio, maktaba, bweni, taaluma, mawasiliano ya moja kwa moja na wazazi pamoja na uwajibikaji wa wafanyakazi. “Shule sasa wanaweza kusimamia mambo ya mahudhurio, maktaba, bweni lakini tuna kipengele cha kutuma mawasiliano kwa wazazi ambapo tumeuunganisha na Whatsapp, Telegram ikiwepo aplikesheni mpya ya simu inayoitwa (shule soft parent Experience) ambapo mzazi atajua kila kitu kinachoendelea shuleni,” amesema Swilla. Pia, ametoa onyo kwa watu wanaoiba kazi za wabunifu nakufanya udanganyifu kwa shule na kuharibu ubunifu wao uliofanyika kwa kutumia jina la taasisi hiyo vibaya na kutengeneza taswira mbaya kwa jamii kwa kujiingizia mapato yasiyo halali. Aidha, ametoa wito kwa wadau wote wa elimu kuungana kufikisha kileleni taaluma ya nchi hii katika viwango vya kimataifa na amewaalika wadau kutoka shule za umma na za binafsi ambazo hazijajiunga na mfumo huo wa shulesoft kufikia ofisi zao zinazopatikana Dar es Salaam, Arusha na Mbeya. Mfumo wa toleo jipya la shulesoft umekusudia kuwaunganisha pamoja utawala wa shule, wazazi, pamoja na Wanafunzi ili kuboresha ujifunzaji katika kipindi hiki cha mageuzi ya sayansi na Teknolojia. Akizungumzia mchango wa uwepo wa Taasisi hiyo katika kuchangiza elimu nchini, Swilla amesema kuwa wameweza kufikia zaidi ya shule 470 nchini ambazo wanafanya nazo kazi na wazazi zaidi ya 200,000. “Pia tuna zaidi ya wanafunzi 200,000 wanaobnufaika na uwepo wa ShuleSoft huku tukifanya shughuli mbalimbali, kwani ukiangalia shule zetu nyingine zimeongeza utendaji kazi na hata ukusanyaji wa mapato umeon, gezeka kutoka wastani wa asilimia 60 hadi 70 lakini kupitia mfumo wetu wa ShuleSoft wameweza kufikia asilimia 90 na zaidi, hivyo mafanikio ni makubwa sana kufikia mfumo huu,” amesema Swilla. Onyo kwa wanaochezea jina Katika hatua nyingine Taasisi hiyo kupitia kwa Mwanasheria wa Taasisi hiyo, Faraja Msuya, imeonya mara moja kwa watu ambao walikuwa wakitumia nembo ya taasisi hiyo kufanya udanganyifu hatua ambayo ilikuwa ikiwarudisha nyuma. Mwanasheria wa Taasisi hiyo, Faraja Msuya. “Baada ya kuwapo kwa watu waliokuwa wakitumia jina letu, tulifungua shauri Mahakama ya Hakimu Kazi Kinondoni na tukashinda kesi, watu hao walijaribu kwebnda mahakama kuu lakini kutokana na sababu za kisheria wahusika hao waliamua kuondoa shauri hilo. “Ifahamike kwamba siyo lengo la Shulesoft kuanza kukimbizana mahaakamlani na mdau yeyote wa elimu, lakini inapofika wakati unalazimisha, hakuna namna. Hivyo tulishinda hiyo kesi, na hatutaki kuendelea kuwa watu wa kesi licha ya kuwapo kwa watu ambao tulisha washinda kisheria lakini bado wanaendelea kudanganya kupitia majina tofautitofauti. “Sasa licha ya onyo ambalo tulikuwa tayari tumetoa wengine walionyesha kukaidi, lakini sijui kama wanafahamu majina ya shule zao kutumika katika shughuli zisizo halali, sasa sisi mwisho wa siku tutalazimika kuchukua hatua kali dhidi yao kwani ni kazi ngumu kutengeneza chapa na kuikuza kisha watu waje waichezee,” amesema Mwanasheria Msuya. Wanaochezea mfumo huo wanafanyaje? Swilla amesema watu wanaochezea mfumo wao, kwanza wamekuwa wakichukua mifumo yao yaliyoanzisha kisha kwenda kwa wateja wakiwaambia kuwa ni wa ShuleSoft. “Watu hao njia moja wanayoitumia kwanza wanakwenda kwa wateja na mfumo wao na kuwadanganya kuwa ni wa ShuleSoft hivyo wanawauzia kwa bei rahisi, hatua ambayo inawasukuma wateja kuona kwamba inapatikana kirahisi licha ya ukweli kuwa kuna kazi kubwa ya kufanya hadi kusimamisha ofisi. “Mbinu ya pili watu hawa wametengeneza nyaraka za uongo wanazopita nazo kwa wateja wetu kisha kuwaambia kuwa ShuleSoft haifanyi kazi tena badala yake kuna kampuni nyingine jambo ambalo siyo kweli, hivyo wanatumia kila mbinu ili kuwashawishi wateja, kwa wateja albao hawajui kuhusu Teknolojia ni rahisi kudanganyika,” amesema Swilla.

YALIYOJIRI KATIKA MKUTANO WA WAZIRI WA ELIMU NA WAZIRI WA ELIMU NA WAMILIKI WA SHULE ZISIZO ZA SERIKALI

event

Katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete, ulioongozwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda, akiwa na TAMISEMI. Mkutano huu ulikua wenye lengo la kupanga mikakati, kutoa changamoto na kuboresha shule binafsi. Yafuatayo ni machache ya yaliyoongelewa; Matumizi ya tehama Wamiliki wa shule zisizo za serikali wamepata kujua umuhimu wa kutumia mfumo wa tehama katika shule zao. Wamiliki hawa wameweza kujua zaidi baada ya kupita kwenye banda la Shulesoft na kupata elimu juu ya mfumo wa kidigitali. Mfumo huu, unasaidia katika kupunguza shughuli za uendeshaji wa shule kwa kuwa na vipengele kama taaluma, uhasibu na mawasiliano. Hivyo kupelekea kuimarisha mahusiano mazuri kati ya shule na wazazi, kupunguza gharama ya uendeshaji shule na kukuza ufaulu wa shule.  Pongezi Wamiliki wa shule binafsi wametoa pongezi zao kwa Waziri, kuita kikao ili kujua shida za shule hizo na kujua namna ya kutatua changamoto hizo. Kodi na tozo mbalimbali Wawakilishi wa wamiliki wa shule walioweza kuongelea swala hili walisema kwamba tozo za huduma na majengo zisamehewe kwani wanatoa huduma ya elimu kama shule za serikali tu ambazo hazitozwi kodi hizi. Pia wanaokuja kwa ajili ya ukaguzi mbalimbali hapo shuleni wameombwa waache kuwawekea vitisho na ukatili kwa wenye shule binafsi mfano zimamoto. Utekelezaji wa sera na mitaala mipya Wamiliki wa shule zisizo za serikali wametoa ombi la kuanzisha masomo ya amali kuanzia madarasa ya awali ili kuwaandaa wanafunzi tangu wakiwa wadogo. Pia wamesema walimu wa masomo haya wanatakiwa waandaliwe ili wawepo kwa wingi kwa ajili ya wanafunzi watakaokuwa wanasoma masomo haya vyuoni.  Maadili  Kati ya maoni yaliyotolewa na wamiliki wa shule zisizo za serikali ni suala la kurudisha somo la dini katika shule na kupewa uzito sawa na masomo mengine. Hii ni kwa sababu wanafunzi hawaipi umuhimu maana somo halijapewa kipaumbele kama mengine kwenye mitihani. Somo hili la dini limeombwa lifundishwe kuanzia madarasa ya awali ili kuwalea watoto katika misingi iliyo bora. Bima Shule za binafsi zimetoa ombi kwa serikali kutafuta namna ya watoto hawa kupata bima ya afya wakiwa shuleni. Hii ni kwasababu shule zisizo za serikali hutegemea mapato kutoka kwa wazazi na pindi mzazi anaposhindwa kulipa ada na huduma nyingine za shule wanafunzi kushindwa kuendelea na masomo kwa sababu shule haiwezi kumudu gharama hizo.  Miundombinu  Maeneo mengi ya shule binafsi zina barabara mbovu kufikia shuleni. Wamiliki wa shule      wametoa ombi kwa serikali kwamba waawasaidie kuwatengenezea barabara zao ili kusadia watu kufikia shule hizo kwa urahisi muda wowote. Waziri akajibu kwa kusema atakaa na viongozi wa maeneo wakati wa kutoa huduma itoe kipaumbele kutoa huduma za umeme,maji na barabara kwenye sehemu za taasisi binafsi na umma. Waziri Mkenda alihitimisha kwa kusema kwamba ameyapokea maoni na malalamiko yote na kuahidi kuyafanyia kazi kabla ya kukutana mwezi Machi mwakani 2024 kupata marejesho ya watakapokua wamefikia. Waziri pia alisema atafanya namna ya kuwapa shule hizi uhuru kwenye utoaji wa ajira na tozo za ada. Pia alitoa pongezi kwa wamiliki wa shule zisizo za serikali kwa kuwa wavumilivu na wakarimu kwake.   Mwisho, Shulesoft inapenda kuwajulisha kuwa tumeweza kuanzisha bima ya wanafunzi wa shule binafsi kwa wanafunzi waliofiwa na mzazi au mlezi, mzazi kuumwa na kushindwa kumhudumia mwanae na ajali inayomkwamisha mzazi kumhumdumia mwanae. Makundi yote haya yanaweza kusaidiwa kufanikisha ndoto zao za elimu kwani bima hii itamsomesha mwanae mpaka atakapomaliza ngazi hio ya elimu. Karibu !!            Kwa maelezo zaidi tupigie +255 748 771 580

Mambo 7 Yaliyojadiliwa Kwenye Mkutano Wa TAMONGSCO -August, 2023

event

1. Ujumbe na mwongozo kutoka kwa REO REO,Bw. Abdul Mnonya alifungua mkutano na kutambulisha meza kuu ya walioalikwa kwenye mkutano huo uliofanyika Oysterbay katika ukumbi wa kanisa la St. Peters.  Pia alitoa mwongozo mzima wa jinsi kikao kitakavyoendeshwa na ratiba nzima ya mkutano. 2. Maelezo ya Msingi Kuhusu Service Levy na Zimamoto Mwanasheria mshauri aliweza kutoa maelezo kuhusu service levy (ushuru wa huduma) kwa wawakilishi wa shule waliokuwepo kwenye mkutano kwamba kwa sasa ushuru ni wa huduma tu na sio wa majengo. Maswali mengi yaliulizwa na maoni yalitolewa kwa mwanasheria huyo ili kufikia muafaka katika eneo hilo. Wawakilishi wa polisi pia waliweza kuwaeleza wenye shule umuhimu wa kufanya ukaguzi wa kushtukiza kwa wanafunzi kuepuka ajali za moto zinazopelekea hasara kubwa kwa shule. 3. Umuhimu wa Kutumia ShuleSoft kwa Shule za Tanzania Eng Ephraim Swilla kutoka Shulesoft alieleza kwa ufupi umuhimu wa programu hii ya shule ambayo imesha ongeza ufanisi mkubwa kwa zaidi ya shule 400 Tanzania nzima zinazotumia mfumo huu. Kwa ufupi Eng. Ephraim Swill alieleza faida zifuatazo Kuongeza ufanisi wa ukusanyaji Ada kwenye Shule Kuboresha na kurahisisha uandaaji wa matokeo kwa wakati kuimarisha mahusiano na wazazi, hivyo kuongeza wigo wa kupata wanafunzi zaidi kuimarisha usimamiaji wa wafanyakazi, kwa kujua ufanisi wao wa kazi kupitia system ya shulesoft kupunguza gharama za uendeshaji wa shule kwa kuondoa ufanyaji kazi wa karatasi Eng. Ephraim alieleza kuwa mfumo wa Shulesoft una moduli zifuatazo   Administration: Hapa Shule wanasajili wanafunzi, wazazi, walimu na wafanyakazi, kuandaa vitambulisho vya wanafunzi na staff, kuandaa ripoti za ufanisi za wafanyakazi (Performance reports), kupata ripoti mbalimbali za wanafunzi n,k. Academic : Hapa shule huweza kusimia mitalaa ya walimu (syllabus), kuandaa matokeo kwenye mfumo kwa dakika chatu tu, shule nzima kupata matokeo na kuwatumia wazazi, kuandaa ripoti za NECTA (CA), kuandaa ripoti za ubora (qualitative reports) etc. Accounts: Hapa shule huweza kuandaa invoice (control number), na kuzituma kwa wazazi, ku record matumizi ya shule (expenses, fixed assets, liabilities etc), kufanya ulinganifu (bank reconciliation), kuandaa mishahara (payroll), etc Communications: Mfumo wa ShuleSoft umeunganishwa na Bulk-sms, Whatsapp, Telegram etc, hivyo kuleta urahisi sana kuwasiliana na wazazi Operations: Hapa shule wanaweza simamia Maktaba, Mahudhurio, ratiba za shule, usafiri etc Digital Learning : Hapa shule wanaweza fundisha wanafunzi pindi wanapokua likizo majumbani, kwani hii sehemu huwezesha shule kurusha vipindi mubarashara, kuweka maswali mtandani, na kuruhu wanafunzi kujisomea wakiwa nyumbani Tazama kwa ufupi ujionee mfumo ulivyo mfumo huu pia unakuja na App special kwa ajili ya mzazi inayoitwa Parent experience Experience. App hii pendwa kwa ma elfu ya wazazi, imekua moja kati ya App bora kabisa Africa, na inatumiwa na wazazi ndani na nje ya Tanzania   Tazama kwa ufupi ujionee App ya wazazi 4. Kuanzisha SACCOSS ya TAMONGSCO Mwenyekiti wa Tamongsco Bw. Amani Lyimo alitoa mapendekezo ya kuanzisha SACCOS kwa ajili ya kikundi hiki cha wenye shule binafsi kuweza kuchangisha wanachama wa Tamongsco ili kuweza kulipia mikutano na kuweza kufanikisha mikutano yao kwa ujumla na kusaidiana. 5. Safari ya China Benki ya NBC na kampuni ya GNM imeweza kufadhili mkutano na kusafiri kwenda China kwa kutoa mikopo ya hadi asilimia 70% kwa watakaoenda nchi hiyo. Madhumuni ya kwenda China ni kujenga mahusiano mazuri na wasambazaji wa bidhaa za shule ili waweze kupata  bidhaa hizo kwa gharama nafuu zaidi. 6. Insurance ya wanachama Kampuni ya Jubilee insurance iliweza kutoa maelezo ya namna wanachama wake wanapata faida kwa kulipia bima hio. Pia Shulesoft pamoja na Sanlam insurance ina kipengele cha bima kinachomsaidia mzazi anapoumwa, kupata ajali au kufariki kuweza kumsomesha mwanao katika kipindi hicho uzuri wa bima ya ShuleSoft, ni kwamba mzazi hulipa kiasi kidogo sana kati ya 10,000 hadi 30,000 kwa mwaka kutokana na Ada ya Shule, na pindi mzazi atapopatwa na changamoto, basi bima italipa ada ya mtoto tangu hilo darasa hadi anapo maliza shule, hivyo kuokoa gharama kwa shule pia 7. Uchaguzi Kulikua na uchaguzi wa viongozi kuwakilisha shule kwa kila wilaya za kanda ya Dar es Salaam na kuweza kutoa matatizo na mrejesho kutoka kwa wanaowakilishwa. Kila wilaya ilifanikiwa kupata viongozi hao na huu ndo ulikua mwisho wa kikao hiki. Kama kuna mengine tumeyaacha, usisite kuyaweka kwenye commnet hapo chini.